Elimu kwa umma

Imewekwa:May 02, 2019

YALIYOJIRI WAKATI WA KIPINDI CHA TUNATEKELEZA KILICHOMSHIRIKISHA AFISA MTENDAJI MKUU WA WAKALA WA VIPIMO TANZANIA WMA DKT LUDOVICK MANEGE APRILI 25, 2019

# Vipimo sahihi ni msingi wa kukua kwa uchumi na ustawi wa wananchi.

# Serikali ya Awamu ya Tano imeiwezesha WMA kutekeleza majukumu yake kikamilifu kwa kuwezesha upatikanaji wa vitendea kazi ikiwemo mizani za kupimia madini kabla hayajasafirishwa nje ya nchi.

# Kuanzishwa kwa Wakala kumekuwa chachu ya wakulima kukuza sekta ya kilimo hapa nchini kutokana na kuwepo kwa vipimo sahihi.

# Moja ya majukumu ya Wakala ni kufanya kaguzi za mara kwa mara ili kuhakikisha kuwa Sheria ya Vipimo inazingatiwa na wadau.

#Serikali imejenga uwezo kwa Wakala kuweza kuhakiki vipimo vinavuotumika katika kipima madini.

#Wakala unahakiki malori ya kusafirisha mafuta yanayopelekwa mikoani na nchi jirani.

# Wakala una vituo vya uhakiki wa malori yanayotumika kusafirishia mafuta.

# Wakala inahakiki pumpu za kuuzia mafuta ili kuona kuwa mchango wa Sekta hiyo unatolewa kama ilivyopangwa na kuchochea ukuaji wa uchumi.

# Serikali ilitupatia kibali cha kuajiri watumishi 100 kwa ajira za muda ili kisaidia kuondoa Changamoto.

# Uchumi wa Viwanda unategemea uwepo wa vipimo sahihi.

.

# Wakala wa Vipimo ni kichocheo cha ukuaji wa uchumi.

# Wakala wa Vipimo ni nyenzo muhimu katika kusimamia Sheria.

#Uwekezaji uliofanywa na Serikali kwa Wakala wa Vipimo ni msingi wa kukuza sekta hii muhimu kwa ustawi wa Taifa.