Dr. Ludovick Manege - Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu

Wakala wa Vipimo (WMA) ni moja wapo ya Wakala za Serikali ambayo ilianzishwa tarehe 13 Mei, 2002 kwa Tangazo la Serikali namba 194 la tarehe 17 Mei,2002. Ambapo hapo awali, kilikuwa kitengo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara na iliongozwa na viongozi mbalimbali.

Miongoni mwa majukumu ya Wakala wa Vipimo ni kuilinda jamii kutokana na madhara yatokanayo na matumizi mabaya ya vipimokatika Sekta za Biashara, Afya, Usalama na Mazingira, Kuthibiti ufungashwaji wa bidhaa, kuwa kiungo kati ya taifa letu na taasisi mbalimbali za kikanda na kimataifa katika masuala ya Vipimo, kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu masuala ya vipimo kwa wadau na kuhakikisha vifaa vyote vitumikavyo nchini kama standards za Vipimo vinaulinganisho sahihi na ule wa kimataifa.