Mfumo wa Kielektroniki wa Malipo ya Serikali (GePG)

TANGAZO

AFISA MTENDAJI MKUU WA WAKALA WA VIPIMO

(WEIGHTS AND MEASURES AGENCY)


ANAUTANGAZIA UMMA KUWA KUANZIA TAREHE 1/7/2018 WAKALA WA VIPIMO ITAANZA KUPOKEA MALIPO KUTOKA KWA WATU BINAFSI AU TAASISI MBALIMBALI ZINAZOPEWA HUDUMA NA WAKALA WA VIPIMO KWA KUPITIA MFUMO MPYA WA KIELEKTRONIKI WA MALIPO YA SERIKALI (Government electronic Payment Gateway)


MALIPO HAYO YANAWEZA KUFANYIKA KUPITIA BENKI ZA CRDB, NMB NA MITANDAO YA SIMU YA M-PESA, TIGO PESA, AIR TEL MONEY AU HALO PESA. BAADA YA KUPATIWA NAMBA MAALUM (CONTROL NUMBER) NA MAAFISA WA WAKALA WA VIPIMO WATAKAOKUWA WAKITOA HUDUMA.


UNAWEZA KUTEMBELEA TOVUTI YETU www.wma.go.tz AU OFISI ZA WAKALA WA VIPIMO AMBAZO ZIPO KILA MKOA ILI KUPATA UFAFANUZI ZAIDI.


KWA MAELEZO ZAIDI TUANDIKIE;


AFISA MTENDAJI MKUU,

WAKALA WA VIPIMO,

NSSF MAFAO, GOROFA YA 7,

MTAA WA UHURU,

S.L.P 313,

DAR ES SALAAM.


BARUA PEPE; info@wma.go.tz


AU TUPIGIE SIMU YA BURE NA; 0800 110097