Ufunguzi wa kituo cha upimaji Misugusugu

WAKALA WA VIPIMO

TANGAZO KWA UMMA

Wakala wa Vipimo inawatangazia wamiliki na wasafirishaji wote wa magari ya mafuta kuwa kituo chetu kikubwa chenye miundombinu ya kisasa kilichopo Mkoani Pwani katika eneo la Misugusugu kitaanza kazi rasmi kuanzia tarehe 1/3/2019.

Kituo hicho kitakuwa na uwezo wa kupima hadi Malori 30 kwa siku badala ya Malori 8 yanayopimwa kwa sasa katika eneo letu dogo lililopo Ilala.

Tunawakaribisha sana kwa ajili ya kuwahudumia.

Imetolewa na;

Wakala wa Vipimo