TANGAZO KWA WAUZAJI WA SARUJI

Wakala wa Vipimo ni Taasisi ya Serikali iliyopo chini ya Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara, ambayo ilianzishwa tarehe 13 Mei, 2002 kwa Tangazo la Serikali namba 194 la tarehe 17 Mei, 2002. Wakala wa Vipimo inatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria ya Vipimo Sura Na. 340.

Sheria ya Vipimo inamkataza Muuzaji wa bidhaa zilizofungashwa kuuza bidhaa zenye uzito pungufu kinyume na ulioandikwa kwenye kifungashio cha bidhaa.

Hivyo, Wakala wa Vipimo inawahimiza wauzaji wote wa Saruji nchini kuwa na mizani sahihi iliyo hakikiwa kwa ajili ya kupima uzito wa mifuko ya saruji wakati wa kupokea kutoka kiwandani ili kuondoa usumbufu unaoweza kujitokeza itakapo bainika kuna mifuko ya saruji yenye uzito pungufu kwenye eneo lako la biashara.

Endapo Mwananchi utabaini kuuziwa saruji yenye uzito pungufu fika kwenye ofisi ya Wakala wa Vipimo iliyopo karibu nawe au wasiliana nao kwa namba ya simu bila malipo 0800 110097 kwa msaada.

Wakala wa Vipimo itaendelea kufanya kaguzi za kushtukiza mara kwa mara na kuchukua hatua za Kisheria kwa watakao bainika kutofuata maelekezo hayo.

IMETOLEWA NA SEHEMU YA MAWASILIANO NA UHUSIANO KWA UMMA.