Ukaguzi wa Mizani kwenye vyama vya Ushirika (AMCOS)

  • Tarehe ya Tukio: May 01, 2022 - May 01, 2022
  • Muda: 08:00
  • Mahali: WMA KAGERA

Wakala wa Vipimo (WMA) kila mwaka kabla ya kuanza kwa msimu wa ununuzi wa Mazao hufanya ukaguzi wa mizani inayotarajiwa kutumika katika ununuzi wa zao la Kahawa. Mizani inayobainika kuwa sahihi uwekewa alama maalumu na Mkaguzi ambayo ni stika ya WMA na mizani yenye kasoro hukataliwa kutumika mpaka ifanyiwe marekebisho na fundi mizani mwenye lesseni kutoka Wakala wa Vipimo na mara baada ya matengenezo Mkaguzi hupita tena kukagua mzani kama upo sahihi unawekewa stika na kukubalika kutumika kununulia mazao.