Afisa Mtendaji Mkuu Bi. Stella Kahwa afanya mazungumzo na Uongozi wa CBE

Imewekwa:August 29, 2023

Afisa Mtendaji Mkuu Bi. Stella Kahwa amekutana na kufanya mazungumzo na Kaimu Mkuu wa Chuo Cha Biashara (CBE) Prof. Tandi Lwoga leo tarehe 29.8.2023.

Mazungumzo hayo yamefanyika katika ofisi za Wakala wa Vipimo Makao Makuu ambapo yamelenga katika kuzidi kuboresha na kuendeleza taaluma ya Vipimo nchini ambapo mpaka sasa kwa Tanzania CBE ndio chuo pekee kinachofundisha kozi ya vipimo na kuzalisha wataalamu wengi kwenye fani hiyo.