DKT. ASHATU KIJAJI ASISITIZA USIMAMIZI WA USAHIHI WA VIPIMO AKIZINDUA BODI YA WAKALA WA VIPIMO (WMA)
Imewekwa:July 31, 2023
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) asisitiza bodi mpya ya ushauri ya Wakala wa Vipimo kuhakikisha walaji wanalindwa kupitia uhakiki wa vipimo ili wanaponunua bidhaa mbalimbali wapate kuona thamani ya fedha katika bidhaa wanazonunua.
Dkt.Kijaji
ameyasema hayo Jijini Dodoma leo tarehe 27 Julai, 2023 alipokuwa anazindua bodi
ya sita ya ushauri ya Wakala wa Vipimo.
Aidha,
amemshukuru Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala pamoja na wajumbe kwa kuaminiwa na kuteuliwa kwani wanaunda timu bora na inayotoa matumaini makubwa katika kuendelea kusimamia
matumizi sahihi ya Vipimo kwenye bidhaa pamoja na vifungashio vyake ili
watumiaji waweze kupata kile walichokilipia. Pia, ameitaka bodi kufanya kazi
yake kwa weledi na kuhakikisha inasimamia usalama wa mali za watanzania kupitia
vipimo sahihi ambapo matarajio ya
Serikali ni kwamba wataisaidia wakala katika kuhakikisha inatekeleza vipaumbele vya
serikali kwenye usimamizi wa matumizi sahihi ya vipimo nchini, na kupitia
usimamizi huo wataweza kuwahudumia wafanyabiashara na wawekezaji na kuishauri serikali kuhusu masuala yote
yanayohusu vipimo na kuhakikisha wakala inamlinda mlaji kwa kutumia vipimo
sahihi Dkt. Kijaji amesema.
Pamoja
na mambo mengine, Dkt. Kijaji ameitaka
wakala kuwa pamoja na kazi nzuri
wanayoifanya ya usimamizi wa vipimo ni vyema kuendelea kuongeza nguvu katika kusimamia usahihi wa vipimo kwenye maeneo mbalimbali
Naye
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Vipimo, Dkt.
Eliza Alfred Mwakasangula alimshukuru Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt.
Ashatu Kijaji (Mb), pamoja na Menejimenti
ya Wakala kwa kuahidi kusimamia na kufanyia kazi maagizo yote yaliyotolewa na
kushauri Wizara ipasavyo kwenye masuala ya vipimo ili kuhakikisha wakala
inaendelea kutoa huduma bora kwa Wananchi inao wahudumia.
Wakati
huohuo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo Bi. Stella Kahwa amemshukuru
Waziri kwa kuteua Bodi ambayo itasaidia kuleta maendeleo kwa wakala, ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya vipimo vinavyohakikiwa kwa
mwaka na kuhakikisha Wakala inaendelea kuchangia katika mfuko mkuu wa Serikali
ili kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi.