Dkt.Ashatu aridhishwa na Maendeleo ya Ujenzi wa Ofisi ya WMA Makao Makuu Dodoma

Imewekwa:August 25, 2023

Dkt.Ashatu aridhishwa na Maendeleo ya Ujenzi wa Ofisi ya WMA Makao Makuu Dodoma.

Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt.Ashatu Kijaji(Mb) ameridhishwa na Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA) chini ya Mkandarasi kutoka Kampuni ya Mohammed Builders Limited.

Dkt.Kijaji amebainisha hayo Agosti 24,2023 alipokwenda kutembelea na kuona maendeleo ya ujenzi wa Jengo la Ofisi za WMA jijini Dodoma.

Aidha Dkt.Kijaji amempongeza Mkandarasi anayejenga jengo hilo kwa kasi nzuri ya ujenzi pamoja na kumtaka kuendelea kufanya kazi kwa kuzingatia mkataba waliokubaliana na Serikali kwani hadi sasa Serikali imetekeleza Jukumu lake la Malipo kama ilivyo kwenye mkataba.

Kwa Upande wa Mkandarasi wa Jengo hilo Ndg.Yusuph Gumbo amesema kuwa hadi kufikia sasa Ujenzi huo umefikia asilimia 70 na unategemewa kukamilika mapema Januari 1,2025.