KAMATI YA BUNGE VIWANDA, BIASHARA, KILIMO NA MIFUGO YAFANYA ZIARA KWENYE MPAKA WA MUTUKULA MKOA WA KAGERA.

Imewekwa:November 23, 2023

Kamati ya Kudumu ya Bunge Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo imeielekeza Wizara ya Viwanda na Biashara kutatuta changamoto za Biashara katika Mpaka wa Mutukula.

Maelekezo hayo yametokewa tarehe 22 Novemba 2023 na Mhe. Deodatus Manyika (Mb) Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo , kwenye ziara ya kutembelea Mpaka wa Mutukula yenye lengo la kuangalia kwa ukaribu utekelezaji wa kazi na majukumu ya Wizara ya Viwanda na Biashara kupitia taasisi zake hususani Wakala wa Vipimo (WMA).
Mhe. Mwanyika Ameeleza kuwa wao kama Kamati kazi yao ni kuisimamia Serikali na kuishauri ili pale penye changamoto hatua zichukuluwe na pale penye mafanikio juhudi ziongezwe zaidi.
"Tumekuja kuangalia kwa ukaribu kama yale yanayotakiwa kufanyika yanafanyika kwa ufanisi pia katika ziara yetu tumebaini changamoto nyingi ,kubwa ikiwa ni ukosefu wa miundombinu ya kutendea kazi na upungufu wa wafanyakiazi" Alisema Mwanyika.
Aidha, amesema kamati imebainia changamoto zote zinazofanya kuwe na mazingira magumu na kuisababishia Serikali kukosa mapato yake , kamati itashughurika nazo ndani ya Bunge na nje ya Bunge.
Kwa upande wake Naibu Waiziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Exaud Kigahe ( Mb) ameishukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo kwa ushirikiano mkubwa ilioutoa katika kutimiza majukumu yake ya kuisimamia na kuishauri Serikali.
"Sisi kama Serikali tunaowajibu wa kuboresha Mazingira ya Biashara Ili kuwe na uharakishwaji wa Biashara (Trade Facilitation) na utoaji wahuduma Ili magari yanayotoka Upande wa Tanzania na Upande wa jirani zetu Uganda yasipate vizuzi vya muda mrefu" Alisema Kigahe
Aidha, Mhe. Kigahe Ameeleza kuwa Changamoto zote zilizoainishwa kwenye mpaka wa Mutukula Serikali itazitafutia ufumbuzi ikiwemo ukosefu watumishi na mashine ya kukagua mizigo (Cargo Scaner) kwa upande wa Tanzania.
Nae Mtendaji wa Forodha Kituo Cha Pamoja Cha Biashara Mtukula ( OSBP) Bw. Steven Joseph Passange amewasilisha taarifa ya utendaji kwenye kamati na kuanisha changamoto kadhaa.
Aidha, Ameeleza kuwa changamoto mbalimbali zinakikabili kituo hicho ikiwemo ukosefu wa mashine ya kukagua mizigo( Cargo Scanner) hali inayosababisha wafanyabiashara kutumia muda mrefu kukagua mizigo yao na kutumia gharama kubwa kwa kuwalipa makuli kufanya kazi hizo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye mpaka wa Tanzania na Uganda Mutukula Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo Bi. Stella Kahwa ameeleza kuwa jukumu kuu la Wakala ni kumlinda mlaji kupitia matumizi sahihi ya Vipimo kwa mujibu wa Sheria ya Vipimo.
Pia, ameeleza kuwa Wakala wa Vipimo ina ofisi katika mipaka mbalimbali Mutukula ukiwa ni Mmoja wa mipaka hiyo ikiwa na lengo la kuhakiki usahihi wa bidhaa zote zinazoingia nchini kupitia mipakani ili kuhakikisha bidhaa zinazoingia zinakuwa sahihi wakati wote kwa lengo la kuwalinda walaji.