MIZANI 1326 IMEHAKIKIWA MTWARA KWENYE MSIMU WA KOROSHO
Imewekwa:October 28, 2022Wakala wa Vipimo Mtwara imefanya uhakiki wa mizani 1326 ili kuhakikisha biashara zinafanyika kwa kutumia vipimo sahihi ili wakulima wa zao la korosho wasipunjike na waweze kunufaika na korosho watakayo uza. uhakiki wa mizani umefanyika katika Wila ya za Newala ambapo mizani 189 imehakikiwa, Tandahimba mizani 332, Mtwara mizani 105, Masasi mizani 344, Nanyumbu mizani 251 na Nanyamba mizani 105.
Mara baada ya kukamilika kwa uhakiki huu ambao kisheria hufanyika mara moja kwa mwaka, maafisa wa Wakala wa Vipimo watapita katika AMCOS mbalimbali ili kujiridhisha kama mizani hiyo inatumika kwa usahihi. Wakala inatoa wito kwa watumiaji wote wa mizani kuhakikisha awafanyi udanganyifu wa kuchezea mizani kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria na yoyote atakayekamatwa atachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa Sheria ya Vipimo Sura Na. 340 na Mapitio yake 2002.
Endapo Mkulima atabaini vitendo vyovyote vya udanganyifu katika mizani wasiliana nasi kupitia namba bila malipo 0800 110097 ama kutembelea ofisi za Wakala wa Vipimo kwa ajili ya msaada zaidi.