ELIMU YA VIPIMO KWA WATU WENYE UHITAJI MAALUM IKWIRIRI, RUFIJI MKOA WA PWANI

Imewekwa:December 28, 2022

Wakala wa Vipimo (WMA) imetoa Elimu ya Vipimo kwa kundi la watu wenye uhitaji maalum ikwiriri kwa lengo la kuwajengea uelewa kuhusu matumizi sahihi ya Vipimo.

Akizumgumza wakati wa ufunguzi Bw. Gaspar Matiku akimuwakilisha Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu amesema kuwa lengo la Wakala wa Vipimo ni kumlinda mlaji kupitia Matumizi sahihi ya Vipimo kwa kufanya uhakiki wa Vipimo mbalimbali ili kuwezesha Biashara zifanyike kwa usawa anayenunua bidhaa apate kwa usahihi kulingana na thamani ya fedha aliyotoa.

Bw. Matiku amewataka washiriki hao wa mafunzo kusikiliza vizuri mafunzo yanayotolewa kuhusu umuhimu wa kutumia Vipimo sahihi ili wakawe mabalozi wazuri katika jamii kwa kusimamia usahihi wa Vipimo.

Amewataka washiriki wa kikao cha elimu kwa Umma kushiriki katika kutoa taarifa kuwaibua wale wanaochezea Vipimo kwa lengo la kuwaibia watumiaji wa Huduma zao kwani kufanya hivyo ni kinyume na Sheria ya Vipimo Sura Na. 340.

Kadharika, amesema taarifa hizo wanaweza kutoa kupitia namba ya Bure ambayo ni 0800 110097 ama kwa kutembelea kwenye Ofisi ya karibu ya Wakala wa Vipimo ili kupata msaada.

Kwa upande wake Afisa Vipimo Mkoa wa Pwani Bw. Isack Birahi akiwasilisha mada amewasihi washiriki hasa wajasiriamali kuzalisha bidhaa zao kwa kutumia Vipimo sahihi na kuandaa vyema vifungashio vya bidhaa zao kwa kuweka taarifa zote za muhimu ili kuongeza thamani ya bidhaa zake ziweze kishindana katika soko la Dunia.

Imeandaliwa na Sehemu ya Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma