WAKALA WA VIPIMO (WMA) YASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA WAFANYA KAZI DUNIANI (MEI MOSI)

Imewekwa:May 01, 2024

WAKALA WA VIPIMO (WMA) YASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA WAFANYA KAZI DUNIANI (MEI MOSI)

Uongozi na watumishi wa Wakala wa Vipimo (WMA), umeshiriki katika maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi),ambapo watumishi wa wakala walijumuika na watumishi wa taasisisi mbalimbali nchini katika maandamano yalifanyika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam.

Katika Maadhimisho hayo, Wakala wa Vipimo imesisitiza kuendelea kufanyakazi kwa ufanisi, weledi na umakini ikiwemo uhakiki wa vipimo mbalimbali ikiwemo Dira zote za Maji huku kauli mbiu ya Wakala ikiwa ni “ Mita za maji za malipo ya kabla zilizohakikiwa na WMA ni suluhisho la ankara za maji”

Maadhimisho ya siku ya wafanya kazi duniani Mei Mosi, yanafanyika kitaifa Jijini Arusha katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid huku mgeni rasmi akiwa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Philip Isdori Mpango akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan ambae awali alitarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo.