Wakala wa Vipimo yaanza kuweka stika maalum katika vipimo mbali mbali vitakavyo hakikiwa
Imewekwa:January 09, 2017Katika jitihada za kuboresha zaidi na kwenda na teknolojia ya kisasa ya kumlinda mlaji katika vipimo, Wakala wa Vipimo (WMA) kwa mwaka huu (2017) itaanza rasmi uwekaji wa sticker katika vipimo vya aina mbalimbali.
1. Uwekaji wa Sticker katika pampu za kuuzia mafuta
Kwa mwaka 2017 itaanza rasmi kubandika
sticker kwenye pampu zinazotumika katika vituo vyote vya mafuta
tutakavyovihakiki, ili mteja ajue uhalali wa kipimo hicho cha mafuta. Kwani
mteja ataona sticker itakayodhihirisha
kituo hicho kimehakikiwa na Wakala wa Vipimo.
2. Kwenye Bohari za Mafuta (Flow
Meters)
Wakala
wa Vipimo pia itaweka sticker maalumu
katika flow meters zinazotumika kujaza
mafuta katika magari ya kubebea mafuta, hivyo wabebaji wa mafuta kwa magari
wataweza kutambua flow meter
iliyohakikiwa.
3. Mizani za Barabarani (Weigh Bridge)
Katika
jitihada za kumlinda mlaji, Wakala wa Vipimo huwa inahakiki mizani zote za
barabarani ili kujua kama mizani hizo zinapima kwa usahihi,
Kwa
mwaka 2017 na kuendelea, kila mzani wa barabarani utakaohakikiwa na Wakala wa
Vipimo utawekewa sticker maalumu ili
muhusika wa gari aweze kutambua mzani uliohakikiwa.
4. Mizani za wafanyabiashara na mizani
zinazotumika viwandani
Mizani
yote ya wafanyabiashara pia uhakikiwa ili kujua usahihi wake.
Aidha, Wakala
wa Vipimo awali tulikuwa tunahakiki mizani na kugonga mhuri wa Serikali katika
mawe na mizani zote za wafanyabiashara na mizani zinazotumika katika viwanda
kwa ajili ya ufungashwaji wa bidhaa, hivyo: kwasasa tutaboresha zaidi, mizani
zote zitakazohakikiwa zitagongwa mhuri pamoja na kubandikwa sticker ambayo itakuwa rahisi kuonekana.
5. Mizani za Kuuzia Mazao ya Wakulima
Katika
jitihada za kumlinda mkulima na mfanyabiashara pia, Wakala wa Vipimo uhakiki
mizani hizo za kupimia mazao ya wakulima (kama vile mazao ya korosho, pamba,
ufuta n.k)
Awali
mizani hizo zilikuwa zinagongwa mhuri wa serikali tu, ila kuanzia January 2017,
kwa kila mzani utakaohakikiwa utagongwa mhuri wa Serikali pamoja na kubandikwa sticker maalumu kutoka Wakala wa Vipimo.
DHUMUNI LA KUANZISHA UBANDIKAJI WA STICKER KATIKA MAENEO TAJWA
- Kwa mlaji itamsaidia kujua uhalali wa kipimo husika, kwani baada ya kubandika sticker na Wakala wa Vipimo mlaji atajiridhisha kuwa mizani anayopimiwa bidhaa au kituo cha mafuta anachohudumiwa kimehakikiwa na mamlaka husika (Wakala wa Vipimo)
FAIDA
- Inasaidia kujua ujazo sahihi wa gari
husika linalosafirisha mafuta, mchanga/ kokoto
- Husaidia walaji kujua kama kipimo kimehakikiwa
au hakijahakikiwa.
WITO
Tunatoa
wito kwa wafanyabiashara wote wanaotumia vipimo, kuhakikisha vipimo vyao vimehakikiwa
na Wakala wa Vipimo na kuwekewa sticker
stahiki,
Sticker hazifanani (kila sticker
ina jina lake kulingana na kipimo) na kila kipimo kina sticker yake.