WAKALA WA VIPIMO YATOA ELIMU KWA BAADHI YA WATUMISHI WA SHIRIKA LA UZALISHAJI MALI JESHI LA KUJENGA TAIFA (SUMA JKT).
Imewekwa:May 14, 2024Katika kuendeleza juhudi zake za kuwafikia wadau na kuwapa elimu ya matumizi sahihi ya vipimo, Wakala wa Vipimo (WMA) imewapa elimu hiyo baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya SUMA JKT waliopo ilala NSSF Mafao leo tarehe 14 Mei, 2024.
Akitoa
elimu katika sehemu ya ofisi za mfuko wa taifa wa hifadhi ya jamii (NSSF) Ilala
Jijini Dar es salaam,Afisa Vipimo Bwana Yahaya Tunda amewaelimisha wafanyakazi
hao namna ya kutambua vipimo sahihi vilivyohakikiwa na Wakala wa Vipimo (WMA) na
matumizi sahihi ya vipimo hivyo katika maeneo mbalimbali ya biashara ili kuleta
haki na usawa kati ya mnunuzi na mtoa huduma.
Bwana
Yahaya ameongeza kuwa, Wakala wa Vipimo inaendelea kujikita katika kutoa huduma
bora sanjari na elimu ya vipimo kwa wadau na wananchi kwa ujumla ili kukuza
ufanisi katika sekta ya vipimo.
Kwa
upande wake msimamizi wa Shirika la Uzalishaji Mali Jeshi la Kujenga Taifa
(SUMA JKT) jengo la NSSF Ilala, Bwana Ernest Baraiga ameishukuru Wakala wa
Vipimo kwa kuwapa elimu na kuwajengea ufahamu juu ya matumizi sahihi ya vipimo
katika maeneo mbalimbali na kuahidi kutoa ushirikiano kwa Wakala katika Nyanja
mbalimbali.
Wakala wa Vipimo kupitia sehemu yake ya mawasiliano na mahusiano kwa umma imekuwa ikitoa elimu na kukutana na wananchi na wadau katika majukwaa mbalimbali ya uelimishaji ili kujenga ufahamu na kutanua wigo wa matumizi sahihi ya vipimo katika maeneo ya biashara,afya,mazingira na usalama na kuleta maendeleo kwa t