YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA BARAZA LA 34 LA WAFANYAKAZI WA WAKALA WA VIPIMO (WMA).

Imewekwa:June 04, 2024

Afisa Mtendaji Mkuu Bw. Alban Kihulla ameongoza kikao cha therasini na nne (34) cha Baraza la Wafanyakazi wa Wakala wa Vipimo kilichofanyika leo tarehe 04.06.2024 katika Ukumbi wa WMA Mkoa wa Kilimanjaro. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Baraza la Wafanyakazi Afisa Mtendaji Mkuu na Mwenyekiti wa Baraza Bw. Alban Kihulla amewapongeza watumishi wote kwa kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kutimiza lengo la usimamizi wa Vipimo kwa ajili ya kuwalinda walaji.

Kadharika, ameahidi kuendelea kuboresha maslai ya watumishi na mazingira Bora ya ufanyaji kazi. Afisa Mtendaji Mkuu amesisitiza watumishi kujiendeleza kielimu kwakuwa kipaumbele namba moja ni elimu ili kuzidi kujiongezea uelewa na kuwahudumia wananchi kwa uweledi.
Kikao cha Baraza la Wafanyakazi kimefanya uchaguzi wa Katibu na Katibu Msaidizi ambapo Bi. Mecktidis Ngonyani amechaguliwa kuwa Katibu wa Baraza akisaidiwa na Bw. Fadhiri Msane kwa nafasi ya Katibu Msaidizi wa Baraza la Wafanyakazi.

Kwa nafasi ya kipekee Baraza la Wafanyakazi limehudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu wa Tughe Taifa Bw. Rugemalira Rutatina ambaye amempongeza mwenyekiti kwa namna ambavyo analiendesha Baraza hilo na kuahidi kutoa mafunzo zaidi kwa viongozi wa Baraza ili kuendelea kuwa na Baraza Bora zaidi.