YALIYOJIRI KWENYE KIKAO CHA WMA NA UONGOZI WA KIWANDA CHA SARUJI CHA DANGOTE

Imewekwa:October 16, 2023

YALIYOJIRI KWENYE KIKAO CHA WMA NA UONGOZI WA KIWANDA CHA SARUJI CHA DANGOTE

Wakala wa Vipimo Makao Makuu imefanya kikao na Uongozi wa kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mkoani Mtwara kwa lengo la kupeana elimu kuhusu matumizi sahihi ya vipimo hususani katika ufungashaji wa bidhaa za saruji zinazo zalishwa kiwandani hapo pamoja na kukagua namna upimaji wa mifuko inayoenda kwa wateja unavyofanyika wakati wa uzalishaji na ufungashaji wa saruji.
Kikao hiki ni muendelezo wa kikao cha awali cha tarehe 15 Septemba, 2023 kilichofanyika baina ya WMA na wazalishaji wa saruji kwenye ofisi za WMA Dar es Salaam.
Uongozi wa kiwanda cha Saruji cha Dangote umeshukuru WMA kwa kutimiza ahadi ya kutembelea kiwanda hicho na kupata uelewa zaidi kuhusu taratibu za ufungashaji wa bidhaa zao na wameahidi kuendelea kutoa ushirikiano wakati wote ili kuhakikisha wateja wao wanaendelea kupata bidhaa zenye Vipimo sahihi.

IMEANDALIWA NA SEHEMU YA MAWASILIANO NA UHUSIANO KWA UMMA WMA