Kurugenzi

Wakala wa Vipimo ina kurugenzi mbili;

  1. Kurugenzi ya Huduma za Biashara
    • Kusimamia kwa usahihi rasilimali za taasisi na kuhusisha matumizi ya Tehama kwa lengo la kutoa huduma bora na kuleta ustawi wa taasisi. Hivyo, Kurugenzi hii;
    • (i) Utoa ushauri juu ya ufanisi wa Taasisi na namna bora ya kuboresha utoaji wa huduma; (ii) Uwezesha Wakala kutekeleza Sera na majukumu ya Kisheria; (iii) Uandaa na kutoa ushauri wa Kitaalam juu ya mifumo ya usimamizi wa fedha na rasilimali za Wakala; (iv) Kusimamia masuala mtambuka yanafanyiwa kazi katika Mpango Mkakati wa Wakala; (v) Kusimamia matumizi mazuri ya fedha na mali za Wakala pamoja na (vi) Kuratibu uandaaji wa Mpango Mkakati na Bajeti katika Wakala.
  2. Kurugenzi ya Ufundi
    • Kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Vipimo Sura Na. 340 na mapitio yake ya mwaka 2002 kwa kuratibu ukaguzi na Uhakiki wa Vipimo vyote vinavyotumika katika Biashara, Afya, Mazingira na Usalama.
    • Kuratibu utekelezaji wa kanuni ya ufungashaji wa bidhaa za Viwandani na mazao ya Kilimo.