Majukumu

Wakala wa Vipimo ina majukumu yafuatayo:

· Kumlinda mlaji katika Sekta ya biashara, afya, usalama na mazingira kupitia matumizi ya vipimo sahihi;

· Kuilinda jamii kuepukana na madhara yatokanayo na matumizi mabaya ya vipimo katika Sekta za Biashara, Afya, Usalama na Mazingira;

· Kusimamia na kutoa ushauri wa kitaalamu kwa wanaojihusisha na utengenezaji, uundaji, na uingizaji wa vipimo mbalimbali katika biashara, afya, usalama na mazingira;

· Kuwa kiungo kati ya Taifa letu na taasisi za kikanda na Kimataifa katika masuala ya Vipimo (Legal Metrology);

· Kuhakikisha vifaa vyote vitumikavyo nchini kama standards za vipimo vinaulinganisho sahihi na ule wa Kimataifa.

· Kukagua na kuhakiki bidhaa zilizofungashwa (Net quantity & labeling);

· Kutoaelimu na ushauri wa kitaalamu kuhusu masuala ya vipimo kwa wadau;