Majukumu ya Wakala wa Vipimo

Wakala wa Vipimo ina majukumu yafuatayo:

  1. Kumlinda mlaji katika Sekta ya Biashara, Usalama, Mazingira na Afya kupitia matumizi ya vipimo sahihi;
  2. Kuilinda jamii kuepukana na madhara yatokanayo na matumizi mabaya ya vipimo katika Sekta ya Biashara, Usalama, Mazingira na Afya;
  3. Kusimamia na kutoa ushauri wa kitaalamu kwa wanaojihusisha na utengenezaji, uundaji, na uingizaji wa vipimo mbalimbali katika Biashara, Usalama, Mazingira na Afya;
  4. Kuwa kiungo kati ya Taifa letu na taasisi za kikanda na Kimataifa katika masuala ya Vipimo (Legal Metrology);
  5. Kuhakikisha vifaa vyote vitumikavyo nchini kama standards za vipimo vinaulinganisho sahihi na ule wa Kimataifa;
  6. Kukagua na kuhakiki bidhaa zilizofungashwa (Net quantity & labeling);
  7. Kutoaelimu na ushauri wa kitaalamu kuhusu masuala ya vipimo kwa wadau.