Kurugenzi
Chunguza kurugenzi mbalimbali zinazoendesha misheni na shughuli za Wakala wa Vipimo.
Kurugenzi ya Huduma za Ufundi
KurugenziKusimamia utendaji kwenye shughuli za utekelezaji wa Sheria ya vipimo
Kutengeneza na kufanya mapitio ya miongozo inayosimamia matumizi ya vifaa na utoaji wa huduma za kiufundi
Kutoa taarifa za utendaji kwenye masuala ya ufundi
Kubuni na kuweka mazingira rafiki ya utoaji wa huduma ili kwenda sambamba na teknolojia mpya za vipimo
Kushiriki kwenye majukwaa ya kikanda na kimataifa yanayohusu vipimo na kusambaza taarifa zake
Kubuni na kuweka mipango ya mwelekeo wa Wakala katika masuala ya ufundi
Kutekeleza majukumu mengine yatakayopangwa na Afisa Mtendaji Mkuu
DIRECTORATE OF BUSINESS SUPPORT
KurugenziKutoa msaada wa kimkakati, kiutawala, na kitaalamu unaolenga kuongeza ufanisi wa taasisi, kuwezesha utekelezaji wa majukumu ya Wakala, kuhakikisha matumizi bora ya rasilimali za fedha na mali, pamoja na kuimarisha upangaji wa kimkakati, bajeti, na ujumuishaji wa masuala mtambuka ili kufikia malengo ya taasisi.
Kutoa ushauri kuhusu ufanisi wa kiutendaji wa taasisi na maboresho ya michakato ya kazi.
Kuwezesha utekelezaji wa sera, mikakati, na majukumu ya Wakala.
Kuanzisha na kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu mifumo ya usimamizi wa rasilimali za fedha na mali za taasisi
Kuhakikisha masuala mtambuka yanajumuishwa na kushughulikiwa katika mipango mkakati ya Wakala.
Kuhakikisha matumizi bora, yenye ufanisi na tija ya rasilimali za fedha na mali za Wakala
Kuratibu mchakato wa upangaji wa kimkakati na uandaaji wa bajeti ndani ya Wakala.