Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wakala wa Vipimo
Vipimo Sahihi na Vya Kuaminika kwa Wote
Background

Uhakiki wa malori ya Mchanga na Kokoto

Maelezo ya kina kuhusu mchakato wetu wa uhakiki.

 Uhakiki wa malori ya Mchanga na Kokoto

Huduma hii inahakikisha kuwa malori yanayosafirisha mchanga na kokoto yanabeba uzito sahihi kulingana na viwango vya biashara. Malori yaliyozidisha mzigo yanaweza kuharibu barabara na kusababisha ushindani usio wa haki. Wakala wa Vipimo hukagua malori haya kwa kutumia mizani ya madaraja na vifaa vya kupimia vilivyohakikiwa ili kuhakikisha yanatii kanuni za uzito

Jinsi inavyofanya kazi

Hatua za Mchakato wa Uhakiki

01

Hatua 1

Malori hupimwa kwa kutumia mizani maalum ya madaraja (weighbridge), na uzito wake huandikwa

02

Hatua 2

Uzito huo unalinganishwa na kiwango halali cha mchanga na kokoto kinachoruhusiwa kusafirishwa

03

Hatua 3

Ikiwa lori limezidisha uzito, marekebisho lazima yafanyike kabla ya kupitishwa

04

Hatua 4

Ikiwa uzito ni sahihi, cheti cha uthibitisho hutolewa