Vitengo
Tazama vitengo maalum vinavyowezesha shughuli zetu na utoaji wa huduma.
Tehama
- Kuandaa na kutekeleza sera, mikakati na viwango vya TEHAMA
- Kujenga, kusimamia na kutunza mifumo, miundombinu na mitandao ya TEHAMA
- Kuhakikisha usalama wa taarifa na upatikanaji endelevu wa mifumo
- Kubuni na kutoa suluhisho za kidijitali zinazosaidia uendeshaji wa shughuli za taasisi
- Kutoa msaada wa kitaalamu wa TEHAMA na huduma kwa watumiaji
- Kuratibu uunganishaji wa mifumo na majukwaa ya Serikali pamoja na wadau mbalimbali.
- Kujenga uwezo wa watumishi kupitia mafunzo na msaada wa TEHAMA
Huduma za Kisheria
- Kinashughulikia na kutoa ushauri wa Kisheria katika mambo yote yanayohusu taasisi
Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini
- Kinahusika na kuratibu shughuli zote za mipango za taasisi
Ununuzi na Ugavi
- Kinashughulikia maswala yote ya ununuzi na ugavi ndani ya taasisi
Ukaguzi wa Ndani
- Kitengo hiki humsaidia Mtendaji Mkuu katika kusimamia mifumo ya uthibiti wa ndani