Uhakiki wa Matanki ya Magari yakubebea vimiminika
Maelezo ya kina kuhusu mchakato wetu wa uhakiki.
Uhakiki wa matanki ya magari ya mafuta unahakikisha kuwa matanki ya mafuta kwenye malori yanakidhi viwango vya kipimo vilivyowekwa. Wakala wa Vipimo hukagua matanki haya ili kuthibitisha uwezo wake wa kuhifadhi mafuta na usahihi wa utoaji wa mafuta. Mchakato huu unahusisha kupitia chati za kalibishaji, kupima ujazo, na kufunga muhuri endapo tanki litathibitishwa kuwa sahihi. Hii huzuia udanganyifu wa mafuta, huhakikisha biashara ya haki, na kulinda watumiaji
Hatua za Mchakato wa Uhakiki
Hatua 1
Wakala hutumia vifaa maalum kupima uwezo halisi wa tanki
Hatua 2
Vipimo vya ujazo hufanyika kwa kujaza tanki kwa kioevu cha kiwango kilichothibitishwa na kuangalia usahihi wake
Hatua 3
Ikiwa tanki litapita uhakiki, linatiwa muhuri na kutolewa cheti cha uthibitisho
Hatua 4
Ikiwa litashindwa, mmiliki anatakiwa kufanya marekebisho na kurudia mtihani wa uthibitisho