Uhakiki wa Pampu za Mafuta
Maelezo ya kina kuhusu mchakato wetu wa uhakiki.
Pampu za mafuta kwenye vituo vya mafuta lazima zitowe kiasi sahihi cha mafuta kwa kila lita. Wakala wa Vipimo huhakikisha kuwa pampu hizi zinatoa kiasi sahihi cha mafuta ili wateja wasipunjwe wanapojaza mafuta.
Hatua za Mchakato wa Uhakiki
Hatua 1
• Vyombo vya kupimia vilivyoidhinishwa hutumika kupima kiasi cha mafuta kinachotolewa na pampu.
Hatua 2
• Ikiwa kiasi cha mafuta si sahihi, pampu lazima ipangwe upya (recalibrated).
Hatua 3
• Baada ya uthibitisho, stika ya uthibitisho inawekwa kwenye pampu.
Hatua 4
• Ukaguzi wa mara kwa mara hufanyika ili kudumisha viwango.