Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wakala wa Vipimo
Vipimo Sahihi na Vya Kuaminika kwa Wote
Background

Uhakiki wa Mizani ya Steelyard

Maelezo ya kina kuhusu mchakato wetu wa uhakiki.

Uhakiki wa Mizani ya Steelyard

Steelyard ni aina ya mizani inayotumika kupima vitu vizito. Inajumuisha beam na mkono unaohamishika, ambao husaidia kubaini uzito kwa kulinganisha na uzito wa kipimo kilichojulikana. Wakala wa Vipimo huhakikisha kuwa Steelyards zikalibishwa kwa usahihi ili kuhakikisha upimaji sahihi wa vitu vizito kama vile bidhaa sokoni au maghalani.


Jinsi inavyofanya kazi

Hatua za Mchakato wa Uhakiki

01

Hatua 1

Wakala hufanya ukaguzi wa Steelyard ili kuhakikisha iko katika hali nzuri na imakalibishwa vizuri. Mkono unaohamishika unakaguliwa kwa ajili ya kufanya kazi ipasavyo, na kipimo cha uzito kinafanywa kwa kutumia uzito wa kipimo kilichojulikana. Ikiwa Steelyard itapita mtihani, itatiwa muhuri na cheti cha uthibitisho kutolewa. Ikiwa itashindwa, inarudishwa kwa mmiliki kwa kalibishaji au matengenezo kabla ya kupimwa tena.