Habari


 • September 06, 2017

  MKUU WA MKOA WA LINDI AHIMIZA MATUMIZI YA VIPIMO SAHIHI

  Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey W. Zambi amewataka Wakala wa Vipimo Kuongeza nguvu zaidi katika kusimamia matumizi sahihi ya vipimo katika maeneo mbalimbali, ili wakulima na Wananchi kwa ujumla waweze kunufaika na mazao wanayolima pindi waendapo kuyauza wakati wa msimu.

  Soma zaidi

 • August 14, 2017

  ZAIDI YA MIZANI 3070 YAHAKIKIWA KATIKA MIKOA YA KANDA YA ZIWA KWA AJILI YA UNUNUZI WA ZAO LA PAMBA

  Wakala wa Vipimo Tanzania ( WMA) chini ya usimamizi wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji imeendelea kutoa elimu kwa wakulima pamoja na kuhakiki mizani itakayotumika kununulia zao la Pamba ikiwa ni maandalizi ya msimu wa ununuzi wa Pamba kwa mwaka huu.

  Soma zaidi

 • August 11, 2017

  JUMLA YA MIZANI 448 YAHAKIKIWA MKOANI MWANZA IKIWA NI MAANDALIZI YA UNUNUZI WA PAMBA

  Wakala wa Vipimo (WMA) Tanzania imeendelea na zoezi la utoaji wa elimu pamoja na uhakiki wa mizani kwenye makampuni mbalimbali ya wafanyabiashara Mkoani Mwanza katika Wilaya za Kwimba, Magu, Misungwi na Sengerema ikiwa ni maandalizi ya msimu wa Pamba.

  Soma zaidi

 • August 11, 2017

  MIZANI 94 KATI YA 150 YATAKIWA KUFANYIWA MAREKEBISHO WILAYANI RUANGWA, MKOA WA LINDI.

  Wakala wa Vipimo nchini imezuia matumizi ya mizani 94 kati 150 ya vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS) katika Wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi, isitumike hadi pale itakapo fanyiwa marekebisho na kuonekana inafaa kwa matumizi.

  Soma zaidi